KISHINDO cha Jokate Mwegelo ni kizito, kimeingia ndani ya uhusiano wa brazameni, Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Wema Sepetu kisha kuwafanya wawili hao kila mmoja kushika hamsini zake.
Wema, amefunga virago, ameondoka nyumbani kwa Diamond, Sinza Madukani, Dar es Salaam kwa mtindo wa “wanakwenu kwa heri, nimechoka masimango, narudi nyumbani kwetu leo.”
Madai ‘yanahiti pointi’ kuwa Diamond na Jokate wapo kwenye penzi jipya lenye nguvu, Wema ameligundua hilo, ameona ni maji marefu, kwa hiyo amejiweka pembeni kuepuka msongamano.
Inazidi kudaiwa kwamba Wema alijaribu kumfanya Diamond atulie lakini ikashindikana, ilipodhihirika Jokate ameshika mpini, alianza kupata mateso ya moyo na hisia kwa jinsi alivyofanywa ‘spea tairi’.
Madai ‘yanahiti’ pia kwamba Wema alithibitisha kuwa Diamond na Jokate wanamchezea ‘ukuti ukuti’ baada ya kuwafumania wakiwa ‘vere klozi’ kimahaba kwenye Hoteli ya Picolo, Masaki, Dar es Salaam.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema alipowakuta Diamond na Jokate, hakuangusha varangati kama mmiliki, badala yake alinywea utadhani yeye ndiye mwizi kisha akawaambia: “Samahanini sana kwa kuwaingilia kwenye starehe zenu.”

VITA YA TANGU ENZI
Wema na Jokate, walipambana kwenye vita ya kuwania Taji la Miss Tanzania mwaka 2006 lakini safari hii wanapambana kwa ajili ya penzi la mwanaume.
Mwaka 2006, Wema aliibuka kidedea kwa kuchukua taji, wakati Jokate alishika nafasi ya pili, safari hii inaonekana kibao kimegeuka, kwani Miss Tanzania huyo bila kulazimishwa, mwenyewe kainua mikono na kutimka.
NENO LA WEMA
Wema akizungumza na paparazi wetu baada ya kurejea nyumbani kwao, Sinza, Mori, Dar es Salaam, alisema kuwa ameondoka kwa Diamond baada ya kujiridhisha kwa ushahidi wa kina kwamba anatoka na Jokate.
Mrembo huyo alisema, anaumia kwa sababu aliamua kutulia na Diamond kwa mapenzi yote na uaminifu, kumbe mwenzake hakuwa na utulivu.
“Unajua watu wengi wanajua mimi situlii na mwanaume mmoja kitu ambacho nakipinga kabisa, kwa maana kuna wakati navumilia ninayofanyiwa na wanaume lakini inashindikana,” alisema Wema.
Staa huyo aliendelea kusema kuwa baada ya kujua uhusiano unaoendelea kati ya Diamond na Jokate, aliamua kujifanya mjinga ili mchumba wake huyo ajirekebishe lakini bado akawa anasikia habari hizo.
“Nimeona bora nirudi nyumbani kwetu nikapumzike kwanza, kwa maana nyumbani kwetu sijafukuzwa wala hakuna shida yoyote,” alisema Wema.
JOKATE NAYE
Jokate alipozungumza na ripota wetu, alisema kuwa hana bifu na Wema kwa sababu hajawahi kumfanyia ubaya wowote.
“Sijatembea na Diamond, nilikuwa karibu naye kikazi. Wimbo mpya wa Diamond unaoitwa Mawazo, video yake na mimi nimecheza.
“Ni kweli kuna maeneo kadhaa nilikuwa naambatana na Diamond lakini siyo kimapenzi. Nilikuwa naye kikazi, siyo kimapenzi hata kidogo,” alisema Jokate.
WOLPER TEH TEH TEHEE!
Kabla ya Jokate kuingilia kati, Wema alikuwa na bifu na staa mwenzake wa filamu, Jacqueline Wolper kwamba ndiye anamuingilia katika mapenzi yake na Diamond.
Bifu hilo, lilikuwa kubwa kutokana na tuhuma kuwa Diamond alianza ‘kukong’ota’ na Wolper kabla hajatua kwa Wema.
Akizungumza na ripota wetu, Shakoor Jongo juzi (Jumatatu), Wolper alisema, ni furaha kwake kubainika kwamba anayemchukua Diamond ni mtu mwingine.
“Mungu Mkubwa, nilikuwa naonekana mimi ndiye tatizo, kumbe adui ni mwingine kabisa, teh, teh, teheeee!” alisema Wolper.
0 comments:
Post a Comment