BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Thursday, October 27, 2011

Mamilioni ya watoto huko Colombia, Iraq, Afghanistan, Uganda, Darfur Sudan, Sierra Leone na katika maeneo mengine mengi kunakojiri vita duniani wameuawa, kujeruhiwa, kupoteza wazazi na jamaa zao na kulazimika kuishi makambini. Ni wazi kuwa asilimia 95 ya wahanga wa migogoro ya kivita ni raia, huku zaidi ya asilimia 80 wakiwa ni watoto na wanawake. Kitendo cha watoto hao kutengana au kuwa mbali na famila zao au kuwa mayatima, kumewalazimisha baadhi yao kubeba jukumu la kuwalea wadogo zao au jamaa zao wakiwa na umri mdogo. Aidha watoto hao hukumbwa na matatizo mbalimbali kama vile kutopata chakula cha kutosha, maji safi na salama, elimu, huduma za afya na usalama.

0 comments: