Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.
Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi. Picha zote na: www.mbeyayetublog.blogspot.com.
Monday, November 14, 2011
Posted by SIRKIWELE at 11:36 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment