BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Friday, November 18, 2011

MOJA KATI YA MAAJABU SABA YA DUNIA


MOJA kati ya maajabu saba mapya yaliyopitishwa duniani hivi karibuni, ni jengo au uwanja uliokuwa ukitumiwa kwa michezo ya mapigano, michezo ya uwindaji wa wanyama, na binadamu kupigana na wanyama kama vile simba na madume ya ng’ombe.

Jumba au uwanja huo uliojengwa enzi za Himaya ya Warumi, katika Italia ya leo, ulikuwa ukiitwa Colesseum au Coliseum.  Mwanzoni  kabisa ulikuwa ukiitwa Flavian Amphitheatre au kwa Kilatini: Amphitheatrum Flavium.

Likijulikana kwa Kiitaliano kama Anfiteatro Flavio au Colosseo), jengo hilo ambalo sehemu kubwa imeharibika na kubaki kama gofu, lilikuwa na umbo la yai na sasa lipo katikati ya Jiji la Rome nchini Italia.

Colosseum lililokuwa na uwezo wa kuingiza watu 50,000 lilijengwa chini ya utawala wa Mfalme Vespasian mwaka 72 Baada ya Kristo (BK) na kumalizika wakati wa utawala wa Mfalme Titus…

0 comments: