BLOGGER TEMPLATES - TWITTER BACKGROUNDS »

Friday, November 18, 2011

MKE MKUBWA AMWONGEZA MUMEWE MAHARI YA MKE WA PILI MORO

Mke mkubwa Bi. Namana Hamis akimkabidhi zawadi mke mwenza, Bi Saida  Hamis Katoto wakati wa ndoa yake na mumewe.
Mke mkubwa akiwa na furaha wakati mumewe na mke mdogo wakifungua muziki siku ya ndoa hiyo.
KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja, Namana Hamis Sombwe, hivi karibuni aliwashangaza watu baada ya kumuongezea pesa ya mahari mumewe, Hassan Omar Kalenga,  aweze kumwona mke wa pili, Bi Saida  Hamis Katoto.

Hili lilitokea karibuni maeneo ya Kigurunyembe, Manispaa ya Morogoro, ambapo baada ya zoezi la ulipaji mahari kukamilika, Kalenga, alifunga ndoa ya pili ya Kiislam na Bi Saida siku ya Ijumaa iliyopita maeneo ya Kihonda Ahmadya.

Hali hiyo iliwashangaza watu ambao wengi waliona halikuwa jambo la kawaida kwa mke mkubwa ‘kushabikia’ ndoa ya mke wa pili.  Ndugu wa bi harusi kutoka Dar es Salaam ndiyo hasa waliokuwa na wasiwasi wa hali kama hiyo ambayo hata hivyo shughuli nzima ilimalizika salama ikiwa ni pamoja na bwana harusi kucheza muziki kwa kuwakumbatia wake zake wote wawili.

Mke mkubwa akipeleka zawadi kwa maharusi.
Mke mkubwa akiwa katika picha ya pamoja na maharusi.
Maharusi wakilishana keki kwa midomo mbele ya mke mkubwa na watoto wa bwana harusi.
Maharusi wakicheza muziki.
Bibi na Bwana harusi wakiaga.

0 comments: