TYYY
HATIMAYE the super business icon ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Abdul Naseeb ‘Diamond’ (pichani chini) ametegua kitendawili cha ‘sapraizi’ yake kwa mpenzi wake Wema Isaac Sepetu kwa kumvisha pete ya uchumba, Risasi Mchanganyiko lina mkoba wenye mafaili yenye kila kitu.
* All News Posts
* My News
* Add
GLOBAL
SHEREHE YA KUVISHANA PETE DIAMOND NA WEMA
* Posted by GLOBAL on October 5, 2011 at 10:00am
* View Blog
Na Musa Mateja
HATIMAYE the super business icon ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Abdul Naseeb ‘Diamond’ (pichani chini) ametegua kitendawili cha ‘sapraizi’ yake kwa mpenzi wake Wema Isaac Sepetu kwa kumvisha pete ya uchumba, Risasi Mchanganyiko lina mkoba wenye mafaili yenye kila kitu.
...Wakilishana keki
Ishu nzima iliyoshuhudiwa na paparazi wetu ilichukua nafasi wikiendi iliyopita, ndani ya ukumbi wa kijanja Bongo, Club Maisha uliopo pande za Masaki, jijini Dar es Salaam katika shoo ya kihistoria iliyopewa jina la ‘Happy Birthday Diamond’ .
.....keki maalumu
Shoo hiyo iliyokuwa na mashabiki kibao, kila mtu alionekana kutaka kujua Diamond atamfanyia nini mpenzi wake huyo baada ya vyombo vya habari kuandika siku hiyo ambayo ni ya kuzaliwa kwake, lakini pia atamsapraizi Wema.
Club Maisha ilikuwa na wakati mgumu, kwani idadi ya watu walioingia katika shoo hiyo ilikuwa kubwa na kadiri muda ulivyozidi kwenda ndivyo wadau walivyozidi kuingia ndani, wengi wakiwauliza waliotangulia kama Diamond ameshakitegua kitendawili cha sapraizi.
ASAFISHIWA NJIA
Kabla ya Diamond kupanda jukwaani na kuonesha ‘sapraizi’ kama alivyoahidi, wasanii kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT) Barnaba Elias na makomandoo kadhaa walipanda jukwaani kwa nyakati tofauti na kupiga shoo safi.
Baadaye, Hemed Suleiman ‘PHD’ ambaye pia anang’ara kwenye muvi za Kibongo, alipanda jukwaani na kuwaonesha mashabiki kwamba yeye ni mkali, kisha aliposhuka Diamond akapanda.
WADAU WAJIACHIA KWANZA KWA KEKI
MC wa shoo hiyo, Hemed Kavu ‘HK’ aliagiza keki imfuate Diamond jukwaani ambapo mashabiki walianza kumuimbia wimbo wa ‘Happy Birthday’ huku shamrashamra zikirindima ukumbi mzima kwa pongezi za msani huyo kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka kadhaa.
0 comments:
Post a Comment